15 JANUARI 2020

15 Januari 2020

Katika Jarida la Habari hii leo Grace Kaneiya anakuletea

-Ripoti mpya iliyotolea na shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu duniani UNFPA inasema hatua za haraka zinahitajika ili kunusuru maisha ya maelfu ya wanawake wajawaziti na watoto wanaozaliwa Darfur Magharibi baada ya kutawanywa na machafuko ya kikabila

-Msimu wa baridi umeelezwa kuongeza madhila zaidi kwa maelfu ya watu Idlib Syria hususan watoto kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF

-Shirika la elimu sayansi na utamaduni la Umoja wa Mataifa UNESCO likishirikiana na shirika la wakimbizi, wadau wengine na serikali ya zambia kwa mara ya kwanza limeendesha zoezi la kuhakiki taaluma za wakimbizi kwenye makazi ya Maheba Zambia na kuwapa paspoti zitakazowawezesha kufanya kazi na kusoma

-Makala yetu leo inatupeleka nchini Uganda kusikia ombi la wakimbizi kwa ajili ya kukuza kipaji cha usanii

-Na mashinani  leo tunapata ujumbe kutoka kwa Bi. Fatima  mkimbizi kutoka Syria mwenye maradhi ya figo ambaye ni mnufaika wa ufadhili binafsi unaowezeshwa na UNHCR.

Audio Credit:
UN News/Grace Kaneiya
Audio Duration:
11'23"

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud