Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari kwa Ujumla

MONUSCO

Waliobakwa DRC wana machungu kiasi cha kushindwa kusimulia ili wasaidiwe

Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC matukio ya ukatili wa kingono ikiwemo ubakaji yanaendelea kutekelezwa kimfumo na vikundi vinavyopigana kwenye taifa hilo lililoshuhudia mapigano mara kwa mara. Flora Nducha na ripoti kamili. 

Mjini Bunia, jimboni Ituri nchini DR Congo, katika ofisi za shirika la kiraia la SOFEPADI, linalosaidia wanawake na watoto waliokumbwa na ukatili wa kingono na ubakaji. 

Sauti
2'24"
MINUSCA/Hervé Serefio

Sasa kutakuwa na amani kati ya wakazi wa Boeing na PK5 mjini Bangui, CAR

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, MINUSCA umejenga kituo cha mafunzo kwa ajili ya vijana wasio na ajira kwenye mji mkuu wa nchi hiyo Bangui, ikiwa ni sehemu ya miradi yake ya matokeo ya haraka, QIPS.  Assumpta Massoi na maelezo zaidi.

Kituo hicho kinalenga vijana wa kata za Boeing na PK5 ambapo wamepatiwa vifaa katika sherehe iliyofanyika kwenye ukumbi wa Bimbo mjini Bangui, mradi ukilenga kuimarisha amani kupitia kuwapatia vijana ajira zenye utu. 

Sauti
1'39"
Arne Hoel/World Bank

UNICEF yasaidia wana Kasese kukabili madhila ya mafuriko

Kutokana na mafuriko ya kila mwaka yanayoikumba wilaya ya Kasese nchini Uganda, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF kwa kushirikiana na serikali ya Uganda, wanaendelea kuimarisha mifumo ya kuhakikisha kunakuwa na mazingira ya kuchukua hatua za haraka kunapokuwa na dharura kama hizo. John Kibego na maelezo zaidi. 

Sauti
1'53"
World Bank/Curt Carnemark

Madini ya risasi yazidi kuharibu ubongo wa watoto duniani- ripoti

Mtoto 1 kati ya 3 duniani kote ana kiwango cha juu cha madini ya risasi kwenye damu yake na idadi kubwa wako nchi za kusini mwa Asia, imesema ripoti mpya iliyotolewa leo na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF na mshirika wake Pure Earth. Flora Nducha na maelezo zaidi.

Huyo ni Nutsa, mtoto mwenye umri wa miaka 9 kutoka Georgia ambaye aligundulika kuwa na kiwango kikubwa cha madini ya risasi mwilini mwake na hata kukatazwa na madaktari kutochezea vikaragosi vya plastiki.

Sauti
2'2"
© UNICEF/Andrea Campeanu

UNICEF inasema COVID-19 imeongeza shida ya watoto wenye utapiamlo

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF limesema kuwa nyongeza ya watoto milioni 6.7 wenye umri wa chini ya miaka mitano wanaweza kupata tatizo la kuwa na uzito mdogo zaidi kulingana na urefu wao na hivyo kuwa na unyafuzi kutokana na madhara ya kiuchumi na kijamii yatokanayo na janga la ugonjwa wa virusi vya Corona au COVID-19.  Flora Nducha na taarifa zaidi.

Sauti
2'37"
TANZBATT 7/Ibrahim Mayambua

Mlinda amani TANZBATT 7 nchini DRC anaeleza ratiba yake ya saa 24

Kila mara tumekuwa tukimulika shughuli za jumla za walinda amani wa Umoja wa Mataifa wanaohudumu katika maeneo mbali mbali duniani iwe ni ujenzi wa barabara, ulinzi wa amani na hata kilimo lakini leo tunaangazia je mlinda amani mmoja mmoja siku yake inakuwa vipi? Na leo tunammulika Luteni Kanali John Ndunguru, Kamanda wa kikundi cha 7 cha Tanzania, TANZBATT 7, kwenye kikosi cha kujibu mashambulizi, FIB cha ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, MONUSCO. Anayetuletea ripoti hiyo ni Issa Mwakalambo, Afisa Habari wa TANZBATT 7. 

Sauti
2'8"