Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

DR Congo

Bukavu, Kivu Kusini. Uchaguzi wa Rais na wabunge umefanyika katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, 20 Desemba 2023.
MONUSCO/Michael Ali

DRC: Maisha yarejea hali ya kawaida huko Fataki, Ituri baada ya mashambulizi kutoka CODECO

Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC kazi ya kuhesabu kura inaendelea baada ya uchaguzi mkuu uliofanyika Jumatano na kuendelea katika baadhi ya maeneo jana Alhamisi, huku ikielezwa kwamba jimboni Ituri, maisha  yamerejea katika hali ya kawaida kwenye eneo la Fataki baada ya mwaka mmoja wa mashambulizi kutoka kwa wanamgambo waliojihami wa kundi la CODECO. 

Sauti
1'20"
Upigaji kura wa kuchagua Rais na Wabunge huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC. Hapa ni Bukavu jimboni Kivu Kusini 20 Desemba 2023
MONUSCO Michael Ali

Uchaguzi DRC: Matokeo ya awali yaanza kubandikwa, wengine walipiga kura leo

Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, matokeo ya awali ya uchaguzi mkuu wa rais, magavana, wabunge na madiwani ambao ulifanyika jana, yameanza kubandikwa katika baadhi ya vituo huku maeneo mengine wapiga kura ambao  hawakuweza kupiga kura kutokana na sababu mbali mbali ikiwemo mvua na kuchelewa kuwasili kwa vifaa wameruhusiwa kupiga kura yao leo Alhamisi. 

Uchaguzi wa rais na wabunge unafanyika katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
MONUSCO/Michael Ali

Uchaguzi mkuu DRC wafanyika kama ilivopangwa

Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, uchaguzi mkuu wa Rais, Magavana, wabunge na madiwani umefanyika hii leo kama ilivyopangwa licha ya changamoto zilizojitokeza katika maeneo mbalimbali ya nchi hiyo. Assumpta Massoi amefuatiliana na kutuandalia ripoti hii. 

Sauti
1'47"
Afisa Habari wa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini DRC, MONUSCO ofisi ya Beni jimboni Kivu Kaskazini akipatia mafunzo wanahabari, wanaharakati na wanafunzi wa Vyuo Vikuu kuhusu habari potofu na habari za uongo mjini Beni.
UN./George Musubao

MONUSCO imetuepusha kutumbukia kwenye usambazaji wa habari za uongo na potofu- Wanufaika

Kesho nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC ni uchaguzi mkuu ikiwa ni tamati ya kampeni huku Umoja wa Mataifa kupitia ujumbe wake wa kulinda amani nchini humo, MONUSCO umeshiriki kwa kusafirisha sio tu vifaa vya uchaguzi lakini pia kuelimisha wananchi jinsi ya kukabili na kuzia habari potofu na za uongo kwani ni tisho la amani na usalama. 

Béatrice Tegbagbo kutoka Bunia mji mkuu wa jimbo la Ituri nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC .
UN News

SOFEPADI imeniondoa kwenye utegemezi - Béatrice

“Nashukuru sana SOFEPADI kwani imenisaidia sana kwenye maisha yangu, hivi sasa naweza kununua chumvi, naweza kununua mafuta,” ni kauli  ya Béatrice Tegbagbo kutoka Bunia mji mkuu wa jimbo la Ituri nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC akizungumza na Idhaa ya Umoja wa Mataifa mjini humo hivi karibuni.