Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Idadi ya majeruhi DRC sasa ni 63, Guterres apaza sauti

Maandamano nchini DRC. Picha: UM/Video capture

Idadi ya majeruhi DRC sasa ni 63, Guterres apaza sauti

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amelaani vikali mauaji ya waandamanaji huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC akisema kitendo hicho hakikubaliki.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amelaani vikali mauaji ya waandamanaji huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC akisema kitendo hicho hakikubaliki.

Yaelezwa kuwa wakati wa maandamano hayo watu 6 waliuawa ilihali idadi ya majeruhi sasa ni 63.

Msemaji wa Umoja wa Mataifa Stephane Dujarric akizungumza na waandishi wa habari mjini New  York, Marekani hii leo amesema..

(Sauti ya Stephane Dujarric)

“Ametoa wito kwa mamlaka za DRC kuchunguza kwa kina tukio hili na kuwajibisha wahusika. Katibu Mkuu amesihi mamlaka za usalama kujizuia na kuzingatia haki za wananchi wa DRC za kuandamana na kujieleza. Ametoa wito pande zote husika kuheshimu maeneo ya ibada.”

Bwana Dujarric amemnukuu Katibu Mkuu kwa mara nyingine tena akitoa wito kwa pande za kisiasa nchini DRC kutekeleza kwa kina makubaliano  ya tarehe 31 disemba mwaka jana…

(Sauti ya Stephane Dujarric)

“Ambayo yamesalia kuwa ndio njia mujarabu ya kufanyika kwa uchaguzi, na kuhamisha madaraka kwa amani na kuimarisha  utulivu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.”