Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watu 6 wauawa DRC, MONUSCO yalaani

Polisi wakikabiliana na waandamanaji mjini Kinshasa, DRC. (Picha:Unifeed video)

Watu 6 wauawa DRC, MONUSCO yalaani

Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC watu sita wameuawa jumapili kwenye mji mkuu Kinshasa wakati wa maandamano yaliyoandaliwa na kanisa katoliki nchini humo. John Kibego na ripoti kamili.

Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC watu sita wameuawa jumapili kwenye mji mkuu Kinshasa wakati wa maandamano yaliyoandaliwa na kanisa katoliki nchini humo. John Kibego na ripoti kamili.

(Taarifa ya John Kibego)

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini DRC, MONUSCO umesema kando ya watu hao 6 waliouawa, watu wengine 56 walijeruhiwa kwenye tukio hilo la polisi kukabiliana na waandamanaji mjini Kinshasa.

Halikadhalika polisi hao wa DRC waliwatia korokoroni watu wengine zaidi ya 100.

Msemaji wa  MONUSCO Florence Marchal ameiambia Radio Okapi kuwa..

(Sauti ya Florence Marchal)

“Baadhi ya watu wetu tuliowatuma kwenda kwenye eneo la tukio ili kufuatialia hali halisi wamekumbwa na vitisho na wengine wamejeruhiwa huku kwenye vitongoji vya Gombe na Lemba. Waandishi wa habari nao wametiwa korokoroni”

Na zaidi ya hapo MONUSCO....

“Tumeshuhudia pia matumizi ya nguvu kupita kiasi”

Hata hivyo msemaji wa polisi amenukuliwa akidai kuwa walichukua hatua kwa kuwa baadhi ya waandamanaji hawakuwa waumini wa katokliki bali wezi ambao walikuwa wanapora mali za watu.

Maandamano hayo yaliitishwa na kanisa katoliki yakitaka kuzingatiwa kwa makubaliano yaliyopitishwa mwishoni mwa mwaka jana kuhusu mchakato wa kisiasa nchini humo.