24 JANUARI 2023
Ni Jumanne ya tarehe 24 mwezi Januari mwaka 2023 ambapo leo tunakwenda nchini Tanzania kuangalia juhudi zinavyofanyika kuhakikisha wanafunzi hususan wa vijijini wanakuwa na mazingira bora ya kuweza kujisomea nyakati zote. Pia tunakuletea habari kwa ufupi zikimulika hali ya usalama DR Congo, ujumbe wa Katibu Mkuu ya siku hii ya elimu duniani na ripoti ya usafirishaji haramu wa binadamu. Katika mashinani tunakupeleka nchini Kenya.