Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Hapa na pale

Watu millioni 2.7 bado wakabiliwa na njaa kali Somalia

Uzalishaji wa chakula pamoja na vyanzo vya mapato vingi nchini Somalia vinatarajiwa kusalia chini kuliko kawaida  katika maeneo mengi nchini humo.

Hii ni kutokana  na uhaba mkubwa wa mvua za msimu za Oktoba- Disemba mwaka 2017 katika maeneo mengi ya Somalia huku mvua za msimu wa April hadi Juni  zikitabiriwa nazo kuwa za kiwango cha chini.

Mvua zinazosaidia uzalishaji chakula nchini humo ni za aina mbili  Deyr na Ga. Msimu wa Deyr hutokea katika miezi ya Oktoba hadi Disemba kila mwaka na  ule wa Ga unaanza  Aprili hadi Juni kila mwaka.

Zahma ya Libya yahitaji dfola milioni 313 mwaka huu

Mratibu wa masuala ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa nchini Libya, amezindua mkakati wa kushughulikia zahma ya kibinadamu mwaka  huu wa 2018 nchini  Libya.

Mpango huo uliozinduliwa na Bi Maria Ribeiro unalenga kuchangisha dola millioni 313 za kutumiwa kwa ajili ya msaada kwa 2018 ili kuokoa maisha ya watu   940,000.

Mpango  mkakati huo (HRP) umezinduliwa kwa niaba ya jumuiya ya wahisani wa misaada ya kibinadamu kwa ushirikiano na wakuu wa mamlaka ya Libya.

Idadi ya majeruhi DRC sasa ni 63, Guterres apaza sauti

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amelaani vikali mauaji ya waandamanaji huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC akisema kitendo hicho hakikubaliki.

Yaelezwa kuwa wakati wa maandamano hayo watu 6 waliuawa ilihali idadi ya majeruhi sasa ni 63.

Msemaji wa Umoja wa Mataifa Stephane Dujarric akizungumza na waandishi wa habari mjini New  York, Marekani hii leo amesema..

(Sauti ya Stephane Dujarric)