Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hofu yaongezeka kwa wanawake na watoto wanaokimbia Cameroon:UNHCR

UNHCR na wadau wake wasajili wakimbizi wa Cameroon wapya wanaosaka hifadhi Nigeria kufuatia machafuko katika maeneo ya lugha ya Kiingereza nchini Cameroon. Picha: © UNHCR

Hofu yaongezeka kwa wanawake na watoto wanaokimbia Cameroon:UNHCR

Wakati idadi ya watu wanaokimbia eneo linalozungumza kiingereza nchini Cameroon na kuingia Nigeria ikiongezeka, Shirika la Umoja wa Mataifa la luhudumia wakimbizi UNHCR linasema hofu yake inaongezeka kufuatia madhila yanayowakabili wanawake na watoto. Assumpta Massoi na taariofa kamili

(Taarifa ya Assumpta Massoi)

Shirika hilo linasema wanawake na watoto ni asilimia 80 ya takribani wakimbizi 10,000 walioorodheshwa Mashariki mwa Nigeria kwenye jimbo la Cross River, huku maelfu ya wakimbizi wengine wa Cameroon katika majimbo mengine bado hawajaandikishwa.

Kwa mujibu wa William Spindler msemaji wa shirika hilo baadhi ya wakimbizi hao ni wavulana na wasichana waliokimbilia Nigeria peke yao, na watoto ambao hawana wazazi au walezi  wanakabiliwa na ugumu wa kupata huduma muhimu kama chakula, kutohudhuria masomo huku ripoti zikisema wanalazimika kufanya kazi na kuwa ombaomba ili waishi na kusaidia familia zao. Ameongeza kuwa

(SAUTI YA WILLIAM SPINDLER)

"Kwa wanawake ukosefu wa ajira ukichanganya na mrundikano kwenye kituo wanachopokelewa wanakuwa katika hatari kubwa ya ukatili wa kijinsia na kingono hususani kuingia katika ngono ili waweze kuishi.”

Hivi sasa UNHCR inashirikiana na serikali ya Nigeria kusaidia kuwaunganisha watoto waliotengana na familia zao, kuwapa ulinzi, na kuhakikisha wanapata huduma muhimu. Pia waangalia eneo la kujenga kambi nyingine ambako wakimbizi watahifadhiwa kulingana na viwango vya kimataifa.