UN ikiadhimisha miaka 80 wakimbizi wasihi kupatikana kwa amani ya kudumu ili warejee makwao
Dunia ikiadhimisha siku ya Umoja wa Mataifa tarehe 24 Oktoba ambapo inatimiza miaka 80 tangu kuanzishwa kwake mwaka 1945 huko San Fransisco nchini Marekani mara baada ya kumalizika kwa vita kuu vya pili vya Dunia ambapo mpaka sasa una jumla ya nchi wanachama 193, wananchi wameomba juhudi zaidi zifanyike ili kumaliza vita na wakimbizi waweze kurejea katika nchi zao.