Watendeeni wema wahamiaji Yemen- UNHCR
Umoja wa Mataifa una wasiwasi mkubwa juu ya madhila yanayokumba wahamiaji, wasaka hifadhi na wakimbizi wapya nchini Yemen. Yaelezwa manusura hufyatuliwa risasi, hupigwa kila mara, hubakwa na hata huvuliwa nguo na kusalia uchi.
Chonde chonde wapeni hifadhi ya kudumu wakimbizi
Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limetoa wito mwingine kwa nchi zilizoendelea kutoa hifadhi ya kudumu kwa wakimbizi na wasaka hifadhi hili kuepusha mafaa zaidi .
Ombi hilo limetolewa leo Genevia kupitia msemaji wa shirika hilo bwana Wiliam Spindler, baada ya vifo vya watu 160, vilivyotokea katika bahari ya Mediteranea mnamo tarehe 8 mwezi huu, wakati mboti walimokuwa wakisafiria kuzama.
Bwana Spindle ameongeza kuwa
(Sauti ya William Spindler msemaji wa UNHCR)
Mikopo yahatarisha maisha ya wakimbizi wa Syria huko Lebanon
Maisha ya wakimbizi wa Syria waliokosaka hifadhi Lebanon yanazidi kuwa hatarini kila uchao, wakati huu ambapo zaidi ya nusu yao ni mafukara.
Hiyo ni kwa mujibu wa mashirika ya Umoja wa Mataifa ikiwemo lile la wakimbizi, UNHCR, la watoto, UNICEF na lile la mpango wa chakula WFP.
Mashirika hayo kupitia utafiti wao yamesema miaka saba ya vita nchini Syria imefanya raia wengi kushindwa kukidhi mahitaji ya maisha yao na baya zaidi ni wategemezi kwa misaada ya kimataifa ambayo nayo haina uhakika.