Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chonde chonde wapeni hifadhi ya kudumu wakimbizi

Wakimbizi wanaowasili katika visiwa vya Lesbos, eneo la kaskazini mwa Aegean huko Ugiriki.(Picha: UNICEF/Ashley Gilbertson VII)

Chonde chonde wapeni hifadhi ya kudumu wakimbizi

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limetoa wito mwingine kwa nchi zilizoendelea  kutoa hifadhi ya kudumu kwa wakimbizi na wasaka hifadhi hili kuepusha mafaa zaidi .

Ombi hilo limetolewa leo Genevia kupitia msemaji wa shirika hilo bwana Wiliam Spindler, baada ya vifo vya watu 160, vilivyotokea katika bahari ya Mediteranea mnamo tarehe 8 mwezi huu, wakati mboti walimokuwa wakisafiria kuzama.

Bwana Spindle ameongeza kuwa

(Sauti ya William Spindler msemaji wa UNHCR)

“Mnamo tarehe 9 Januari , wajumbe wa UNHCR na washirika wetu ambao ni shirika la kimataifa la kutoa  huduma ya Afya, la (Medic Corp) walisaidia katika zoezi la kuwpokea  wahamiaji wapatao 279 waliookolea na vikosi vya uokoaji vya Libya kwenye pwani ya Libya. Waathirika waliripoti kuwepo kwa watu kati 60 na 100 ambao wamepotea baharini.”

Bwana Spindler amesema walipata taarifa kwama vikosi vya uokoaji  Moroco vilifanikiwa kuokoa zaidi ya watu 54, halikadahlika uokozi mwingine kutoka vikosi vya ukokoaji vya Italy ulinusuru maisha ya wahamiaji 60 katika baharí ya mediteranea.

UNHCR inaendelea na wito kwa nchi  ya tatu kutoa nafasi ya hifadhi ya kudumu kwa wakimbizi wakimbizi 40,000 ambao baadhi yao walipelekwa kwenye kambi ya mpito Niger baada ya matukio ya vitendo vya kikatili mwaka jana vya baadhi ya wahamiaji kuuzwa kama watumwa huko Libya.