Cameroon

Cameroon - Siku nzima na mchuuzi Christine Banlog

Christine Banlog amekuwa mchuuzi kwa miaka 22 sasa. Yeye ni mjane mwenye umri wa miaka 64, na sasa analea wajukuu wake watatu huko Nyalla, kitongoji cha mji wa Douala nchini Cameroon.

Programu ya UNICEF ya elimu kwa njia ya redio yaokoa watoto wakimbizi Cameroon

Kuelekea siku ya radio duniani tarehe 13 mwezi huu wa Februari, tunakwenda nchini Cameroon ambako mradi wa mafunzo ya elimu kwa njia ya redio yamekuwa jawabu kwa maelfu ya watoto waliofurushwa makwao kutokana na ghasia kwenye maeneo ya kusini-magharibi na kaskazini-magharibi mwa nchi hiyo..

Sauti -
2'1"

11 Februari 2021

Hii leo Jaridani Grace Kaneiya kutoka Nairobi Kenya anaanza Habari za UN akimmulika msichana kutoka Rwanda ambaye ni mhandisi wa magari kwenye kampuni ya magari ya Hyundai kwenye mji mkuu Kigali, ikiwa ni katika maadhimisho ya siku ya kimataifa ya wanawake na wasichana katika sayansi.

Sauti -
13'38"

Radio yawa jawabu la elimu kwa watoto wakimbizi Cameroon

Kuelekea siku ya radio duniani tarehe 13 mwezi huu wa Februari, tunakwenda nchini Cameroon ambako mradi wa mafunzo ya elimu kwa njia ya redio yamekuwa jawabu kwa maelfu ya watoto waliofurushwa makwao kutokana na ghasia kwenye maeneo ya kusini-magharibi na kaskazini-magharibi mwa nchi hiyo.

Maelfu waendelea kufungasha virago CAR na kuingia Cameroon kusaka usalama:UNHCR

Watu zaidi ya 5,000 wamefungasha virago siku za karibuni wakikimbia mashambulizi ya waasi nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR hasa kwenye mji wa Magharibi wa Bouar na kuingia nchi jirani ya Cameroon kusaka usalama, limesema shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR.

Ninalaani kitendo hiki cha kutisha, kilichoua na kujeruhi watoto-Henretta Fore 

Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la Umoja wa Mtaifa la kuhudumia watoto UNICEF, Henrietta Fore  amelaani vikali shambulizi ambalo limetekelezwa jana na kuua wananchi wakiwemo watoto katika mji wa Mozogo, kaskazini mwa Cameroon. 

UNHCR yatiwa hofu na wanaokimbia ghasia CAR

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR limesema lina hofu kubwa ya kwamba ghasia na ukosefu wa usalama vitokanavyo na uchaguzi mkuu wa tarehe 27 mwezi uliopita nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR, vimesababisha zaidi ya watu 30,000 kukimbilia nchi jirani za Cameroon, Chad, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) na Jamhuri ya Congo.
 

Buriani walindaamani wetu:MINUSCA

Umoja wa Mataifa kupitia mpango wake wa kuweka utulivu nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati,

Sauti -
2'42"

Hifadhi ya Dja Cameroon yachukua hatua kupambana na COVID-19 

Maeneo mengi ya hifadhi za viumbe hai na misitu pamoja na mbuga za wanyama pori yameathirika kwa namna moja au nyingine kutokana na uwepo wa mlipuko vya virusi vya corona ulimwenguni. Hifadhi ya Dja nchini Cameroon ni miongoni mwa waathirika, lakini ambao wanafanya chini juu kujikinga na kujikwamua na hali hiyo.

UN yashtushwa na kulaani mauaji ya raia Cameroon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres ameelezea kushtushwa kwake na ripoti ya kwamba shule moja kwenye mji wa kumba kusini magharibi mwa Cameroon ilishambuliwa tarehe 24 mwezi huu huu na watoto kadhaa kuuawa.