Walinda amani wanapogeuka mabwana mifugo Sudan Kusini

17 Januari 2018

Kikosi cha jeshi la India kilichoko  mkoa wa Malakal Sudan Kusini, kama sehemu ya kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa kimetoa msaada wakutibu mifugo ya wafugaji wa eneo la Akola,lililoko umbali wa kilomita sitini na tano, kaskazini mashariki mwa mji mkuu wa jimbo hilo.

Kikosi cha jeshi la India kilichoko  mkoa wa Malakal Sudan Kusini, kama sehemu ya kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa kimetoa msaada wakutibu mifugo ya wafugaji wa eneo la Akola,lililoko umbali wa kilomita sitini na tano, kaskazini mashariki mwa mji mkuu wa jimbo hilo.

Wakati wa shughuli hiyo wafugaji walieleimishwa  kuhusu magonjwa  kadhaa yanayoshambulia mifugo katika eneo hilo na njia gani za kufuatwa ili mifugo yao iwe salama, hivyo ufugaji uwe wa manufaa katika upatikanaji wa chakula na kuwepo kwa amani ya kudumu.

Mabwana mifugo wa kikosi cha India waliweza kushughulikia mifugo zaidi ya 500 ambao baadhi walipewa dawa za kuua minyoo na magonjwa mengine.

Mabwana mifugo ni sehemu ya kikosi kikubwa  cha jeshi la India katika maeneo ya Upper Nile ambacho kina wataalamu wengi kama vile wahandisi ambao kwa sasa wanakarabati barabara ndefu ya umbali  wa kilomita 205 inayotumiwa kwa misaada  kati ya Malakal na Melut. Hatua yao hii inasaidia  juhudi muhimu za kikosi cha UNMISS za kuhakikisha amani ya kudumu katika nchi hiyo.

Tayari wakaazi wa Akole wamesha faidika na kazi za wahandisi wa kikosi hicho .Hii ni kutokana na hali kubadilika kuwa sawa kufuatia eneo hilo kuwa halipitiki kutoka Malakal kwa sababu ya mvua kali za mwezi juni mwaka jana ambazo ziliharibu daraja muhimu katika barabara hiyo.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa UNGA76 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter