Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Pambaneni na magonjwa ya kilimo na mifugo: FAO

Wadudu waharibifu wa mimea kwenye matawi ya mahindi. Picha: FAO

Pambaneni na magonjwa ya kilimo na mifugo: FAO

Kuna uhitaji wa haraka wa kuongeza mapambano ya wadudu  waharibifu wa mimea na magonjwa yanayoenea hasa maeneo ya mipakani na kuathiri mifugo na mimea.

Imeeleza taarifa ya tathmini iliyotolewa wakati wa kikao cha shirika la chakula na kilimo duniani, FAO kilichokutanisha wawakilishi kutoka nchi zaidi ya 20 na mashirika mengine ya kilimo na wanyama huko Roma, Italia.

Wadudu hao ni viwavi jeshi,  pamoja na ugonjwa wa mnyauko wa migomba na ugonjwa unaosumbua zaidi kondoo na mbuzi au PPR.

FAO imetolea mfano  viwavi jeshi ikisema wadudu hao wanapatikana zaidi katika nchi za Afrika zilizo kusini mwa jangwa la Sahara na iwapo hawatadhibitiwa watasababisha hasara ya dola bilioni 4.8 kwa zaidi ya wakulima milioni 200

Tayari FAO kwa kushirikiana na mashirika mengine imetoa programu ya miaka 5 ya kujikinga na kupambana na wadudu na magonjwa hayo, programu ambayo inahitaji dola milioni 98.