FAO yaanza kampeni ya chanjo ya mifugo milioni 9.4 kote nchini Sudan
Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo Duniani (FAO), kwa kushirikiana na Serikali ya Sudan, limezindua kampeni ya kitaifa ya chanjo ya mifugo kwa mwaka 2025 ili kulinda maisha na riziki za wafugaji na wakulima wanaokadiriwa kuwa zaidi ya milioni tatu kote nchini Sudan, ambao wanakabiliwa na janga kubwa la uhaba wa chakula.