Ulevi na matumizi ya dawa za kulevya inaathiri afya, pata usaidizi uondokane nazo
Ripoti iliyotolewa jana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ulimwenguni WHO imesema mamilioni ya vifo vinachangiwa na unywaji pombe na matumizi ya dawa za kulevya na imetoa wito wa haraka wa kutekeleza lengo namba 3.5 la Malengo ya Maendeleo Endelevu SDG la kupunguza matumizi ya pombe na dawa za kulevya na kuboresha upatikanaji wa matibabu bora kwa matatizo ya matumizi ya dawa.