Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Upper Nile

09 APRILI 2025

Hii leo jaridani tunaangazia hali ya kibinadamu katika katika jimbo la Upper Nile nchini Sudan, na haki za binadamu na watu kutoweka kwa wingi nchini Sudan. Makala inatupeleka nchini Kenya na Mashinani tunakwenda Gaza, kulikoni?

Sauti
12'9"
Wasichana wananawa kwenye kisima cha maji katika kambi ya watu waliokimbia makazi yao huko Bentiu, Sudan Kusini.
© UNICEF/Mark Naftalin

Raia wanapaswa kulindwa kwa njia zote vita ikishika kasi Sudan Kusini: OCHA

Ghasia zinazoendelea katika kaunti za Nasir, Ulang, na Baliet, Jimbo la Upper Nile nchini Sudan Kusini zimeathiri vibaya jamii za eneo hilo na shughuli za kibinadamu, na kusababisha watu takriban 50,000 kukimbia makazi yao tangu mwishoni mwa mwezi Februari,amesema Mratibu wa Masuala ya Kibinadamu wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini, Bi. Anita Kiki Gbeho katika taarifa iliyotolewa na Shirika la Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Misaada ya Dharura, OCHA  leo mjini juba, nchini Sudan Kusini, na kuonesha wasiwasi mkubwa kuhusu hali hiyo, akiwataka wahusika wote kuheshimu raia, wahudumu wa misaada, na miundombinu muhimu.

18 MACHI 2025

Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Kenya kumulika elimu ya mtoto wa kike kama moja ya nguzo muhimu katika jamii ukizingatia malengo endelevu ya maendeleo ya Umoja wa Mataifa.Pia tunakuletea muhtasari wa habari na sauti za mashinani.

Sauti
11'24"
© WFP/Eulalia Berlanga

UNMISS: Wananchi wa kaunti ya Nasir watakiwa kuepuka mapigano ili wapelekewe maendeleo

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Sudan Kusini (UNMISS) umewaeleza wananchi wa Kaunti ya Nasir au Keich Kon iliyoko jimboni Upper Nile nchini Sudan Kusini kuwa ili waweze kurejeshewa huduma za misaada ya kibinadamu ni vyema wakafikia makubaliano ya kusitisha mapigano. 

UNMISS pamoja na wadau wengine wa misaada ya kibinadamu walifikia uamuzi wa kusitisha huduma zao katika kaunti ya Nasir kutokana nae eneo hilo kutofikika na pia ukosefu wa usalama uliosababishwa na mapigano ya mara kwa mara baina ya wanajamii wa kuanti hiyo, na pia mapigano na kaunti za jirani.

Sauti
1'56"
© WFP/Hugh Rutherford

UNMISS: Uongozi wa jimbo la Upper Nile nchini Sudan Kusini waomba usaidizi zaidi wa ulinzi

Huku mzozo wa Sudan ukiendelea, wakimbizi na wanaorejea wanamiminika katika mipaka ya nchi jirani ya Sudan Kusini, wengi wamekuwa wakitafuta hifadhi katika jimbo la Upper Nile nchini humo na wanahitaji msaada wa haraka wa kibinadamu.  Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini UNMISS umefanya mazungumzo na uongozi wa jimbo hilo kuona namna ya kuwasaidia. 

Sauti
2'25"