Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNMISS na mbinu bunifu ya kulinda raia Sudan Kusini

Walinda amani katika Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini, UNMISS. Picha: UM/JC McIlwaine

UNMISS na mbinu bunifu ya kulinda raia Sudan Kusini

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini, UNMISS unatumia mbinu mpya na nafuu zaidi ya kuimarisha ulinzi kwa raia kaskazini-mashariki mwa nchi hiyo.

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini, UNMISS unatumia mbinu mpya na nafuu zaidi ya kuimarisha ulinzi kwa raia kaskazini-mashariki mwa nchi hiyo.

Mbinu hiyo mpya inatumika kwenye mji wa Akobo, kaskazini-mashariki mwa nchi hiyo ambako walinda amani wanapiga doria za hapa na pale na kuzunguka badala ya kujenga kituo cha kudumu cha ujumbe huo.

Mji huo huo uko kwenye maeneo yanayoshikiliwa na wapinzani wa serikali ya Sudan  Kusini.

Viongozi wa eneo hilo pamoja na raia waliuomba Umoja wa Mataifa kutuma huko walinda amani na sasa jeshi hilo limeitikia mwito huo na mwelekeo mpya wa kuwepo kwa askari wa kupokezana zamu badala ya kuwepo kambi ya muda mrefu.

Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini na pia mkuu wa UNMISS David Shearer amesema mbinu hii inatumia rasilimali kidogo na wataweka miundombinu muhimu ya kusaidia kikosi hicho kinachopokezana zamu.