Chuja:

Malakal

UN Photo/Isaac Gideon

Malakal Sudan Kusini watumia bendi ya muziki inayoeneza amani

Mpango wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini, UNMISS, wanashirikiana na washirika wake wa amani, watu wa Sudan Kusini, kuleta sauti zinazotetea amani ya kudumu katika nchi mpya zaidi ulimwenguni lakini inayoendelea kuteseka na migogoro, vifo na kutawanywa, miaka kadhaa tangu vita ya wenyewe kwa wenyewe. John Kibego na maelezo zaidi.

Ni watoto wa Sudan Kusini wakiwa wameshikilia gitaa kila mmoja, wamekalia viti vya kamba, kila mmoja amevaa barakoa wanafuata kwa umakini maelekezo ya mwalimu wao wa muziki. 

Sauti
2'14"
UN

UNMISS yasaidia Upper Nile kuchukua hatua kusongesha amani

Nchini Sudan Kusini kwenye jimbo la Upper Nile, mkutano ulioitishwa na ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo kwa lengo la kurahisisha utekelezaji wa mkataba mpya wa amani umezaa matunda na hivyo kuleta nuru katika utokomezaji wa ukatili wa kingono na usambazaji misaada ya kibinadamu.
Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini, UNMISS ulichukua hatua ya kuleta pamoja magavana wa jimbo la Upper Nile na makamanda waandamizi kwa lengo la kuona jinsi gani ya kutekeleza mkataba huo mpya wa amani wa mwaka 2018 kwenye jimbo hilo.

Sauti
2'7"