Mapigano ya kikabila Sudan Kusini yachochea hali ngumu- Lacroix
Gharama ya mzozo wa Sudan Kusini kwa wananchi inazidi kuongezeka kila uchao wakati huu ambapo mapigano yanaendeleo huku mahitaij ya kibinadamu nayo yakiongezeka.
Mkuu wa operesheni za ulinzi wa amani kwenye Umoja wa Mataifa Jean-Pierre Lacroix amesema hayo hii leo akiwasilisha ripoti ya siku 90 ya Katibu Mkuu wa umoja huo kuhusu hali ya usalama na kibinadamu nchini Sudan Kusini.
(Sauti ya Jean-Pierre Lacroix)
Kinachoongeza zaidi athari kwenye usalama ni mapigano ya kikabila. Mfano wa pekee zaidi ni tarehe 28 mwezi novemba ambapo watu wapatao 45 waliuawa, 19 walijeruhiwa na mamia waliona nyumba zao zikitekezwa kwa moto wakati kikundi cha Murle waliposhambulia kijiji cha wadinka huko Jonglei.”
Bwana Lacroix hata hivyo akagusia pia mjadala wa kitaifa unaofanyika Sudan Kusini kuchambua vyanzo vya mzozo akisema..
(Sauti ya Jean-Pierre Lacroix)
“Kwa maelezo mengi, mashauriano hayo yamekuwa ya dhati na yameibua hofu sahihi kabisa za umma kuhusiana na uongozi, rushwa na utawala wa kisheria. Hata hivyo wasiwasi uliopo ni kwa jinsi gani matokeo yake yatatumika »