Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Guterres alaani mashambulizi ya kigaidi Baghdad leo

Katibu mkuu Antonio Guterres. Picha: UM

Guterres alaani mashambulizi ya kigaidi Baghdad leo

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amelaani vikali mashambulizi mawili ya kigaidi yaliyoptokea leo mjini Baghdad nchini Iraq.

Kupitia taarifa iliyotolewa na msemaji wake, Katibu Mkuu ametuma salamu za rambirambi kwa familia za waathirika wa mashambulizi hayo na kuwatakia ahuweni ya haraka majeruhi. Watu zaidi ya 20 wamedaiwa kuuawa na wengine wengi kujeruhiwa.

Guterres amerejea kusema kwamba Umoja wa Mataifa utaendelea kushikamana na serikali na watu wa Iraq katika juhudi za kupambana na ugaidi na kulijenga upya taifa hilo.