Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM walaani shambulizi la kigaidi Baghdad

Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Iraq, Ján Kubiš. Picha; UM/Amanda Voisard

UM walaani shambulizi la kigaidi Baghdad

Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Iraq,  Ján Kubiš  amelaani  vikali shambulio la kigaidi lililotokea usiku wa kuamkia leo kwenye mji mkuu Baghdad na kusababisha vifo vya raia  12 na kujeruhi wengine wengi.

Bwana Kubis metuma salamu za rambirambi kwa wafiwa na pia serikali ya Iraq huku akiwatakia ahueni  majeruhi.

Pia ameitaka serikali ya Iraq ifanye uchunguzi kubaini wahusika ili wachukuliwe hatua za kisheria haraka iwezekanavyo.

Aidha Bwana Kubis ameonya serikali ya Iraq kuwa  ingawa ISIL wameshindwa na  majeshi ya Iraq bado wataendelea kuwa tishio  kwa maisha ya wananchi  wa Iraq kila uchao.