Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Dola milioni 187 zahitajika kwa usaidizi Ukraine- Walker

Mapigano Ukraine yanaendelea kuharibu miundombinu muhimu, na raia wahitaji misaada. Picha (Maktaba): UNHCR_Iva Zimova

Dola milioni 187 zahitajika kwa usaidizi Ukraine- Walker

Mwakilishi mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Ukraine Neal Walker amesema dola milioni 187 zinahitajika kukidhi mahitaji ya kibinadamu nchini humo kwa mwaka 2018.

Amesema hayo mjini Geneva, Uswisi wakati akihutubia wawakilishi wa nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa wakati huu ambapo wananchi milioni 2.3 wanahitaji misaada ya dharura.

Bwana Walker amesema kiasi mzozo huko mashariki mwaka Ukraine ukiingia mwaka wa nne. wananchi hawawezi tena kujikimu na wanalazimika kuchagua cha kugharimia kati ya chakula, dawa, malazi, matibabu au elimu ya watoto wao.

Amekumbusha kuwa ingawa mzozo wa Ukraine unasahaulika, bado wanawake, wanaume, vijana, watoto na wazee wanaendelea kupata machungu ikiwemo kukabiliwa na mashambulizi ya makombora wakati wakivuka vituo vya ukaguzi kwenda kusaka huduma muhimu.

Mwakilishi huyo wa Umoja wa Mataifa nchini Ukraine amesema bila kupatikana kwa fedha hizo, watoa misaada ya kibinadamu watashindwa kutoa huduma hasa wakati  wa majira ya baridi kali.