Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Umoja wa Mataifa Tanzania wapeleka kampeni ya #ZuiaUkatili huko Kigoma

Kampeni ya #ZuiaUkatili huko Kigoma nchini Tanzania. Picha: UN Women Tanznaia

Umoja wa Mataifa Tanzania wapeleka kampeni ya #ZuiaUkatili huko Kigoma

Siku 16 za kupinga ukatili dhidi ya wanawake zikiwa zikiendelea kuangazia maeneo mbalimbali duniani, nchini Tanzania hii leo Umoja wa Mataifa umepeleka kampeni hiyo huko mkoani Kigoma, Magharibi mwa nchi hiyo. Taarifa zaidi na John Kibego.

(Taarifa ya John Kibego)

Kampeni hii imetumia njia mbalimbali kupitisha ujumbe wa kuzuia ukatili dhidi ya wanawake na watoto wa kike ambapo miongoni mwa mbinu hizo ni ngoma hii ya asili ikiporomoshwa na watu wazima ambao ni wanawake kwa wanaume wa wilaya ya Kibondo, mkoani Kigoma.

Afisa kutoka shirika la masuala ya wanawake la Umoja wa Mataifa, UN-Women nchini Tanzania Lucy Tesha akaelezea kile wanachofanya kupitia programu maalum kwa mkoa wa Kigoma.

(Sauti ya Lucy Tesha)

Naye mwakilishi mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Tanzania Alvaro Rodriguez kupitia kidokezo cha kampeni ya Zuia Ukatili dhidi ya wanawake anasema..

(Sauti ya Alvaro Rodriguez)