Skip to main content

Chuja:

unyanyasaji wa kijinsia

Mjane raia wa Sudan Kusini ambaye mume wake aliuawa siku moja baada ya yeye kujifungua mtoto wao wa mwisho sasa ndio pekee anaihudumia familia yake
WFP/Gabriella Vivacqua

UNMISS yaendesha mafunzo ya kukabiliana na unyanyasaji wa kijinsia

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Sudan Kusini UNMISS umeendesha mafunzo ya kukabiliana na unyanyasaji wa kijinsia ikiwemo ubakaji katika eneo la makutano la  Aru jimboni Equatoria ya Kati ikiwa ni njia mojawapo ya kuwaandaa wananchi kujilinda kwa kuwa vita vya wenyewe kwa wenyewe vimekuwa vikijirudia na kuathiri zaidi wanawake na wasichana. 

Umoja wa Mataifa unafanya kazi na jamii Kavumu, DRC kwa ajili ya kuelimisha watu kuhusu ukatili wa kijinsia.(Picha ya maktaba)
MONUSCO/Alain Likota

Walionyanyaswa kijinsia washukuru Mfuko wa UN kufadhili miradi yao Kavumu, DRC  

Miaka sita iliyopita, yaani mwaka 2016, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa aliunda Mfuko wa kufadhili miradi inayolenga kusaidia waathirika wa unyanyasaji wa kijinsia na hata watoto waliozaliwa kutokana na ukatili wa kingono uliofanywa na baadhi ya wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa wakiwemo walinzi wa amani au watu wengine wanaohusika na shughuli za Umoja wa Mataifa katika mataifa mbalimbali. 

Mtoto mkimbizi kutoka Ukraine amesimama na mbwa wake kwenye kituo cha wakimbizi cha muda karibu na kivuko cha Palanca kwenye mpaka wa Jamhuri ya Moldova na Ukraine, tarehe 26 Februari 2022.
© UNICEF/Constantin Velixar

Nina wasiwasi kuhusu kuongezeka kwa unyanyasaji wa wanawake na wasichana nchini Ukraine: Pramila Patten

Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu kuhusu Unyanyasaji wa Kijinsia katika Migogoro, Pramila Patten, ana wasiwasi mkubwa kuhusu hali inayozidi kuzorota nchini Ukraine na ametoa wito wa haraka wa ulinzi wa raia, hasa wanawake na wasichana, ambao wameathiriwa kwa kiasi kikubwa na migogoro ya kivita na kukimbia.

03 Desemba 2021

Karibu kusikiliza jarida hii leo tukikuletea mada kwa kina kutokea nchini Tanzania kuhusu mapokeo ya uamuzi wa serikali kuwarejesha shuleni watoto waliokatiza masomo kwa sababu mbalimbali ikiwemo  ujauzito.

Pia utasikia habari kwa ufupi zikiangazia siku ya Kimataifa ya watu wenye ulemavu ambayo ni leo na ujumbe wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa siku hii pamoja na habari kutoka Afghanistan na Ethiopia. 

Sauti
12'25"
© UNICEF/Vinay Panjwani

Ripoti ya UNFPA yaonesha takribani nusu ya wanawake wote katika nchi zinazoendelea, wananyimwa uhuru wao wa mwili

Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu, UNFPA iliyotolewa leo Aprili 14, 2021, takribani nusu ya wanawake wote katika nchi 57 zinazoendelea wananyimwa haki ya kuamua kuhusu miili yao kama vile tendo la ndoa, uzazi wa mpango au kutafuta huduma za afya. Taarifa ya Anold Kayanda inaeleza kwa kina.

Sauti
4'42"
UN Women

Tulikuwa tunawapiga wake zetu lakini elimu imetubadilisha - Wanaume Dodoma.

Ripoti ya hivi karibuni ya shirika la afya la Umoja wa Mataifa iliyoandaliwa kwa ushirikiano na wadau, imeonesha kuwa mwanamke 1 kati ya 3 sawa na wanawake milioni 736 wanakumbwa na unyanyasaji kama vile vipigo na ukatili wa kingono kutoka kwa wapenzi wao au wanaume wasio wapenzi wao na idadi ya matukio imeonekana kuwa ya kiwango cha juu katika muongo uliopita. Kwa hivyo, Umoja wa Mataifa umeendelea kuhamasisha jamii kote ulimwenguni kuondokana na unyanyasaji wa namna hiyo na aina nyingine zozote za unyanyasaji. Katika hali inayoonekana kuunga mkono wito wa Umoja wa Mataifa, nchini Tanzania

Sauti
4'4"