UN-Tanzania imefanya mengi kutuelimisha kuhusu SDGs- Rahma
Wiki hii katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani limefanyika kongamano la kimataifa la vijana la mwaka 2018, lenye lengo la kuwajumuisha vijana katika malengo ya maendeleo endelevu au SDGs.
Tulipata fursa ya kukutana na mmoja wa washiriki wa jukwaa hilo Rahma Abdallah Mwita ambaye ni kijana kutoka Tanzania. Rahma ni mmoja wa wanzilishi wa mtandao wa vijana kuhusu mabadiliko ya tabianchi ( Youth Climate Change Activist Network).