Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Habari Mpya

Mhudumu wa afya akifunga bandeji kwenye mguu wa mtoto katika hospitali moja huko Gaza.
© WHO

HABARI KWA UFUPI: Gaza, Ukraine, Uchumi

Kwa mujibu wa shirika la afya la Umoja wa Mataifa duniani WHO na timu yake iliyoko katika ukanda wa Gaza, idadi ya vifo na majeruhi kutokana na mzozo unaoendelea baina ya Israel na kundi la Hamas inaongezeka kila uchao na waathirika wakubwa ni wanawake na watoto. Akitoa takwimu katika mkutano na waandishi wa habari mjini Geneva Uswis hii leo mwakilishi wa WHO kwenye eneo linalokaliwa la Palestina Dkt. Rik Peeperkorn amesema “Kutokana na takwimu za wizara ya afya ya Gaza tunazungumzia zaidi ya watu 23,000 waliokufa ambapo asilimia 70 ni wanawake na watoto, takriban watu wengine elfu 59 wamejeruhiwa ambao ni asilimia 2.5 ya watu wote, na asilimia 3.5 ya watu wote wameathirika moja kwa moja.”

Francis Njoroge, Mkulima kutoka Muranga nchini Kenya.
IFAD

Mkulima Kenya: Mradi wa IFAD umenisaidia baada ya kuathiriwa na mabadiliko ya tabianchi

Mradi wa kilimo endelevu unaofadhiliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Kilimo, IFAD na Serikali ya Kenya ambao unalenga kukuza miche ya miti na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi umeleta manufaa kwa wakulima wadogo kutoka eneo la Kaunti ya Kiambu nchini Kenya na kuboresha ukulima wao. Mkulima mdogo Francis Njoroge ni mmoja wa mamilioni ya wakulima wadogo wanaokabiliwa na athari za mabadiliko ya tabianchi lakini kwa bahati nzuri, amefaidika na Mfuko wa Upper Tana Nairobi Water Fund unaolenga kukuza miche ya miti na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

Sauti
4'4"
Watu waliojeruhiwa wakisubiri kutibiwa katika hospitali ya Al Shifa mjini Gaza. (Maktaba)
© WHO

Mzozo Gaza: Hospitali zazidi kuzidiwa uwezo, wagonjwa sakafuni

Ikiwa leo ni siku ya 93 tangu mapigano yaanze huko Ukanda wa Gaza kati ya jeshi la Israel na wanamgambo wa kipalestina waliojihami, likiwemo kundi la Hamas, mashirika ya Umoja wa Mataifa ya usaidizi wa kiutu yanazungumzia uwepo wa idadi kubwa ya vifo miongoni mwa wanawake na watoto huku yakisihi timu za madaktari ziruhusiwe kuingia eneo la Gaza ili ziendelee na jukumu la kuokoa maisha. 

Sauti
2'16"