Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wanasayansi wa IAEA waanza utafiti wa athari za taka za plastiki Antaktika

Wanasayansi wa IAEA waanza utafiti wa athari za chembechembe za taka za plastiki Antaktika
UN Photo/Mark Garten
Wanasayansi wa IAEA waanza utafiti wa athari za chembechembe za taka za plastiki Antaktika

Wanasayansi wa IAEA waanza utafiti wa athari za taka za plastiki Antaktika

Tabianchi na mazingira

Shirika la kimataifa la nguvu za atomiki IAEA kwa kushirikiana na serikali ya Argentina leo wamezindua utafiti wa kwanza wa kisayansi kuchunguza uwepo wa chembechembe za taka za plastiki Antaktiki kama sehemu ya juhudi za kukabiliana na changamoto inayoongezeka ya kimazingira hata katika maeneo ya mashambani na mbali zaidi ya nchi ya dunia.

Rais wa Argentina, Javier Milei, na Mkurugenzi Mkuu wa IAEA Rafael Mariano Grossi walijiunga na timu ya wanasayansi ya IAEA kwenda katika vituo vya Antaktika vya Marambio na Esperanza Argentina kuashiria kuanza kwa operesheni yao. 

Waziri wa ulinzi wa Argenyina Luis Petri, waziri wa mambo ya ndani Guillermo Francos na waziri wa mambo ya nje Diana Mondino pia walikuwepo. 

Timu ya watu wawili ya utafiti kisha itaanza kwa mwezi mmoja kutathmini athari za chembechembe za plastiki kwa kuchunguza kutokea na usambazaji wake katika maji ya bahari, maziwa, kwenye mchanga, mchanga, maji yanayotiririka na wanyama wa mfumo wa ikolojia wa Antaktiki karibu na kituo cha utafiti wa kisayansi cha Argentina Carlini.

Mradi wa IAEA wa NUTEC

Operesheni ya IAEA kwa Antaktika, bara la kusini zaidi duniani, unatekelezwa kupitia mpango wa plastiki wa NUTEC wa IAEA. 

NUTEC ilianzishwa mwaka wa 2020 na ni mpango mkuu wa IAEA kupambana na uchafuzi wa plastiki kwa kutumia teknolojia ya nyuklia. 

Kupitia mtandao wa maabara ya ufuatiliaji wa plastiki ya NUTEC, mbinu za nyuklia na isotopiki zinatumiwa kutoa takwimu kuhusu usambazaji wa chembechembe za plastiki baharini kwa kuchukua sampuli na kuchambua kuenea kwa chembechembe hizo za plastiki katika mazingira. 

Takwimu hizi sahihi za kisayansi zinawakilisha taarifa muhimu kwa ajili ya kuunda hatua na sera za kukabiliana na plastiki na utupaji wake.

Ushahidi wa taka za plastiki Antaktika

Ushahidi wa kwanza wa uwepo wa chembechembe za taka za platiski za chini ya kipenyo cha mm 5 mm zilipatikana katika barafu ya pwani ya Antaktika mwaka 2009 wakati watafiti kutoka chuo kikuu cha Tasmania walipopima sampuli ya barafu ya bahari huko Antaktika Mashariki. 

Lakini bado hakuna taarifa inayopatikana kuhusu wapi na ni kiasi gani cha plastiki hufika Antaktiki na ni kiasi gani kinachukuliwa na viumbe vya Antaktiki. 

Pia kuna takiwmu ndogo sana zilizopo kuhusu aina za chembechembe za plasiki zinazofikia eneo hili safi kupitia mikondo ya bahari, utuaji wa angahewa na uwepo wa binadamu katika eneo hilo la Antaktika.

Katika hafla ya kuzindua operesheni hiyo tarehe 6 Januari katika Uwanja wa Marambio wa Antaktika nchini Argentina, Mkurugenzi Mkuu wa IAEA Grossi alisema kuwa ugunduzi wa cjembechembe za taka za plastiki katika mazingira ambayo hapo awali hayajaguswa ya Antaktika hutumika kama ushuhuda wa ushawishi wa uchafuzi unaoenea na hatari. 

“Chemvechembe za plastiki ni tatizo la kimataifa, lakini jumuiya ya kimataifa bado haina takwimu za kisayansi zinazohitajika kufanya maamuzi sahihi. Hili ndilo lengo la mradi wa plastiki wa NUTEC, kwa kuelewa asili ya plastiki, harakati na athari, tunaweza kufanya maamuzi sahihi juu ya jinsi ya kushughulikia tatizo hilo”.

Athari za chembechembe za plastiki Antaktika

Kwa mujibu wa IAEA uwepo wa chembechembe za plastiki unaweza kuchangia kuongeza kasi ya upotevu wa barafu huko Antaktika kwa kupunguza utengenezaji wa barafu, kubadilisha uso wa barafu, kukuza shughuli za vijidudu, kufanya kazi kama vihami joto, na kuchangia kudhoofisha muundo wa barafu. 

Shirika hilo limeongeza kuwa changamoto hizo zinapojumuishwa na mabadiliko ya tabianchi, hali ya anga, na athari za bahari, uwepo wa chembechembe za plastiki utaongeza athari mbaya ya kuyeyuka kwa barafu katika Antaktika. 

Kwa kuongeza kwa chmbecheembe za plastiki zinazoingia kwenye mlolongo wa chakula wa viumbe vya Antaktiki huathiri vibaya afya ya maisha ya Antaktiki na mnepo wao kwa mabadiliko ya tabianchi.