Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Volker Türk: Mamlaka DRC zishughulikie kauli za chuki

Wakazi wa Kisangani wajitokeza kwa wingi kupiga kura katika uchaguzi wa kitaifa 2023
Idhaa ya Umoja wa Mataifa
Wakazi wa Kisangani wajitokeza kwa wingi kupiga kura katika uchaguzi wa kitaifa 2023

Volker Türk: Mamlaka DRC zishughulikie kauli za chuki

Haki za binadamu

Kamishna Mkuu wa Haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Volker Türk ameeleza wasiwasi mkubwa kuhusu kuongezeka kwa kauli za chuki zenye misingi ya kikabiila na uchochezi wa ghasia nchini Jamhuri ya Kidemokrasia Kongo DRC. 

Katika taarifa yake iliyotolewa hii leo jijini Geneva Uswisi Kamishna Mkuu huyo ameeleza kuongezeka kwa kauli hizo hasa katika majimbo ya Kivu Kaskazini na Kivu Kusini na pia katika mikoa ya Kasaï na Katanga, baada ya uchaguzi mkuu wa mwezi uliopita.

 “Kauli za chuki, za kudhalilisha utu na za uchochezi ni za kuchukiza na zinaweza tu kuongeza mvutano na vurugu katika nchi ya DRC yenyewe, pamoja na kuweka usalama wa kikanda katika hatari.” Amesema Kamishna Türk.

Ameeleza kutambua juhudi za baadhi ya mamlaka dhidi ya tabia hiyo, lakini amesisitiza hatua kali zaidi zinahitajika kuchukuliwa.

“Natoa wito kwa mamlaka kuchunguza kwa kina na kwa uwazi ripoti zote za kauli za chuki na uchochezi wa vurugu na kuwawajibisha waliohusika.”

 

Soma hapa kuhusu uchaguzi Mkuu nchini DRC na matokeo ya awali.