Msaada unaoingia Gaza hautoshelezi matakwa ya watu milioni 2.2: Jamie McGoldrick
Katika mahojiano maalum na UN News kupitia njia ya simu yaliyofanyika kutoka Jerusalem leo Januari 13 Jamie McGoldrick, Naibu Mratibu Maalum wa Muda na Mratibu Mkazi, wa Ofisi ya Mratibu Maalum wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya mchakato wa amani ya Mashariki ya Kati UNSCO, amesema, "kuna hali ya mshtuko na kiwango cha kukata tamaa. Na nadhani kuna hali ya kutokuwa na tumaini huko pia, kwa sababuwatu wa Gaza hawaoni hatua yoyote kwa kile wanachokikabili mbele yao.”