Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vita dhidi ya Hamas huko Gaza ni kitendo cha kujilinda, Israel yaiambia mahakama ya ICJ

Mikutano ya hadhara katika kesi ya Afrika Kusini dhidi ya Israel katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki
ICJ-CIJ/ Frank van Beek
Mikutano ya hadhara katika kesi ya Afrika Kusini dhidi ya Israel katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki

Vita dhidi ya Hamas huko Gaza ni kitendo cha kujilinda, Israel yaiambia mahakama ya ICJ

Amani na Usalama

Israel imekanusha vikali shutuma kuwa ina nia ya mauaji ya kimbari dhidi ya Wapalestina na kusisitiza kuwa ipo katika vita ambayo wao hawakuianzisha na wala hawakuitaka kufuatia hapo jana nchi ya Afrika kusini kuwasilisha kesi mbele ya mahakama ya Umoja wa Mataifa ya kimataifa ya haki ICJ wakitaka kukomesha mauaji ya raia huko Gaza. 

Leo ijumaa ya tarehe 12 Januari ni siku ya pili na ya mwisho ya kusikilizwa kwa kesi ya awali katika Mahakama ICJ ambapo baada ya jana Afrika Kusini kusisitiza hoja ya mauaji ya kimbari dhidi ya Wapalestina, leo timu ya wanasheria wa Israel imesisitiza kwamba wana malengo mawili ambayo mosi ni kutokomeza tishio lililokuwepo la wanamgambo wa Kipalestina wa Hamas na Pili ni kuwaachilia huru mateka 136 ambao bado wanashikiliwa katika vita inayoendelea huko mashariki ya Kati. 

Mahakama ya Kimataifa ya Haki, ICJ inasikiliza kesi ya Afrika Kusini dhidi ya Israel.
ICJ-CIJ/ Frank van Beek
Mahakama ya Kimataifa ya Haki, ICJ inasikiliza kesi ya Afrika Kusini dhidi ya Israel.

Kamanda wa Israel Tal Becker aliwaambia majaji wa ICJ huko The Hague nchini Uholanzi kuwa “Israel iko katika vita dhidi ya Hamas, sio dhidi ya watu wa Palestina” kufuatia mashambulizi ya kigaidi yaliyoongozwa na Hamas tarehe 7 Oktoba mwaka 2023. 

Akisoma jumbe za mwisho zilizotumwa na baba wa moja ya familia za wakulima ambao nyumba zao zilichomwa moto na watu wanaodhaniwa kuwa ni Hamas, Bwana Becker amesema “kumekuwa na mateso ya kiraia "ya kutisha" na "ya kuhuzunisha moyo" "katika vita hivi, kama katika vita vyovyote vile.”

Becker pia amekataa ombi la Afrika Kusini kwa mahakama chini ya vifungu vya Mkataba wa Mauaji ya Kimbari la kutoa "hatua za muda" ili kuiamuru Israel kusimamisha mara moja shughuli zake za kijeshi huko Gaza akisema kuwa hatua hiyo ni “jaribio la kuinyima Israel uwezo wake wa kutimiza wajibu wake wa kuwalinda raia wake, mateka, na zaidi ya Waisraeli 110,000 waliokimbia makazi yao ambao hawakuweza kurejea kwa usalama makwao,”

Tweet URL

Wanasheria wa Israel wamewaeleza majaji wa ICJ kuwa nchi inaposhambuliwa, ina haki ya kujilinda yenyewe na raia wake, 

“Hakuna nia ya mauaji ya kimbari hapa, haya sio mauaji ya halaiki,” wakili wa Israel Malcolm Shaw aliiambia mahakama hiyo akisisitiza kuwa ukatili uliofanywa na wanamgambo wa kipalestina wa Hamas “hauhalalishi ukiukwaji wa sheria katika wakujibu mashambulizi na bado ni chini ya mauaji ya halaiki - lakini unahalalisha...utekelezaji wa haki halali na ya asili ya Nchi kujilinda kama ilivyoainishwa katika Mkataba wa Umoja wa Mataifa”.

Timu ya wanasheria wa Israel pia imekataa maelezo yaliyowasilishwa hapo jana na timu ya wanasheria ya Afrika kusini ikisema yana “upotoshaji sana” na kwamba wanatumia neno “Mauaji ya kimbari” kama silaha ambapo Wakili Galit Raguan aliiambia mahakama hiyo kuwa “Vita vya mijini daima vitasababisha vifo vya kusikitisha, madhara na uharibifu, lakini huko Gaza matokeo haya yasiyotakikana yanazidishwa kwa sababu ni matokeo yanayotarajiwa ya Hamas.”