Elimu na Amani: Wakimbizi waelezea jinsi elimu ilivyobadili mtazamo wao hasi dhidi ya watu wengine
Nafasi ya elimu katika kuchagiza amani miongoni mwa wakimbizi na jamii zinazowahifadhi imedhihirika huko Uganda wilayani Kikuube magharibi mwa nchi ambako kuna makazi ya wakimbizi ya Kyangwali. Hilo limethibitika wakati huu dunia kesho Januari 24 ikiadhimisha siku ya elimu duniani maudhui yakiwa kujifunza kwa ajili ya amani.