Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mashirika ya UN yanasaidia DRC kukabiliana na mafuriko

Baadhi ya uharibifu wa mazingira na mali uliofanywa na mafuriko huko Kalehe, jimboni Kivu Kusini, DRC mwezi Mei, 2023. (Maktaba)
UN News/George Musubao
Baadhi ya uharibifu wa mazingira na mali uliofanywa na mafuriko huko Kalehe, jimboni Kivu Kusini, DRC mwezi Mei, 2023. (Maktaba)

Mashirika ya UN yanasaidia DRC kukabiliana na mafuriko

Msaada wa Kibinadamu

Mashirika ya kibinadamu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia Kongo DRC yaeleza hali ya mafuriko nchini humo bado ni mbaya ambapo karibu nusu ya majimbo 26 ya nchi hiyo ikiwemo mji mkuu wa Kinshasha yameathiriwa na mafuriko makubwa.

Taarifa iliyotolewa hii leo na msemaji wa Umoja wa Mataifa Stéphane Dujarric, jijini New York Marekani imenukuu mamlaka DRC kuwa zaidi ya kaya 400,000 zinahitaji msaada wa dharura, ikiwa ni pamoja na chakula, malazi na msaada wa afya.

Mratibu wa Misaada ya Kibinadamu nchini humo, Bruno Lemarquis, alitembelea jamii zilizoathirika mjini Kinshasa wiki iliyopita na kueleza wasiwasi wake mkubwa kuhusu hali ya maisha katika maeneo hayo kuwa ni hatarishi. 

Baadhi ya familia zinaishi katika nyumba zao ambazo bado zimejaa mafuriko, na hivyo kuongeza hatari ya kupta maonjwa yanayosababishwa na maji, ambayo yanaweza kuzidisha hatari katika mfumo wa huduma ya afya ambao tayari una matatizo.

Nini Kinafanyika 

“Sisi na washirika wetu tunafanya kazi kwa karibu na mamlaka ya Kongo kuunda mpango wa kukabiliana na dharura na kupunguza mzozo wa afya ya umma.” Amesema Dujarric,

Mashirika ya kibinadamu yanatoa msaada wa dharura kama vile huduma za afya kwa waliojeruhiwa na kutekeleza hatua za kuzuia hatari ya milipuko na magonjwa.

Pia Umoja wa Mataifa unafanya kazi kwa bidii, kusaidia mashirika ya ndani kufanya tathmini.

Mashariki mwa DRC 

Walinda amani wa Umoja wa Mataifa wanaendelea kulinda njia kuu za usambazaji zinazoelekea Goma na Sake, huko Kivu Kaskazini. 

Walinda amani hapo pia wanasaidia jeshi la Kongo kuzuia kundi la waasi la M23 kusonga mbele kuelekea Sake na Goma.

Msemaji huyo wa UN amewajulisha waandishi wa habari kuwa wanajeshi wa kulinda amani na wanajeshi wa Kongo wametumwa huko Masisi, Rutshuru na Nyiragongo, kushika doria katika maeneo muhimu.

“Misheni pia ilianzisha eneo la ulinzi karibu na kituo chake cha Kitchanga ili kusaidia kulinda wanaume, wanawake na watoto wapatao 25,000 wanaotafuta makazi kutokana na ukosefu wa usalama ambao tumekuwa tukiuzungumzia.” 

Uwepo wa walinda amani pia unawezesha utoaji wa misaada ya kibinadamu kwa wale wemue unitage.