Hofu ya uhalifu wa kivita yatanda baada ya Israel kuvamia Rafah
Hatua yoyote ya Israel kuendeleza uvamizi wake kamili wa Gaza hadi katika mji wa kusini wa Rafah wenye msongamano mkubwa wa watu inaweza kusababisha uhalifu wa kivita ambao lazima uzuiwe kwa gharama yoyote, imesema leo ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu misaada ya dharura OCHA.