Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari kwa ufupi: Kipindupindu; Miradi ya afya; Ukeketaji

Mtoto mvulana akipokea chanjo ya kipindupindu nchini Haiti. (Maktaba)
© PAHO-WHO/David Spitz
Mtoto mvulana akipokea chanjo ya kipindupindu nchini Haiti. (Maktaba)

Habari kwa ufupi: Kipindupindu; Miradi ya afya; Ukeketaji

Afya

Idadi ya wagonjwa wa kipindipindu hususan Mashariki na kusini mwa Afrika imeongezeka mara mbili mwaka huu ikilinganishwa na mwaka jana ambapo jumla ya wagonjwa 26,000 na vifo 7000 vimeripotiwa katika wiki nne za mwanzo wa mwaka huu kutoka nchi 10 zikiongozwA na Zambia na Zimbabwe.

Akizungumza na waandishi wa habari kwa njia ya mtandao huko Geneva Uswisi, Meneja wa operesheni za dharura wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ulimwenguni -WHO kanda ya Afrika Dkt. Fiona Baraka amezitaja nchi nyingine kuwa ni “ Msumbiji, Tanzania, Jamhuri ya Kidemokrasia Kongo, Ethiopia na Nigeria. Hizi ni nchi zilizo kwenye hatari ya kusambaza ugonjwa huu kwa nchi nyingine.” 

Miongoni mwa sababu ya idadi hiyo kubwa ya vifo ni unyanyapaa ambapo watu wengi hawaendi vituo vya afya hivyo WHO inashirikiana na nchi husika kutoa elimu kwa umma.

Halmashauri kuu ya UNITAID katika Hospitali ya Kaunti Ndogo ya Ruiru ikikutana na wadau wa hospitali wa wakuzaji afya ya jamii. Wanaunganisha wagonjwa katika jamii na huduma za VVU, TB, na Malaria wanapoambukizwa, na kuwapatia msaada katika kufuatilia ma…
UNITAID Kenya
Halmashauri kuu ya UNITAID katika Hospitali ya Kaunti Ndogo ya Ruiru ikikutana na wadau wa hospitali wa wakuzaji afya ya jamii. Wanaunganisha wagonjwa katika jamii na huduma za VVU, TB, na Malaria wanapoambukizwa, na kuwapatia msaada katika kufuatilia mawasiliano na huduma za nyumbani ili kuhakikisha wagonjwa wanfuata maagizo wakianza regiments zao.

Miradi ya afya Kenya

Nchini Kenya Bodi ya shirika la Umoja wa Mataifa la kufanikisha upatikanaji wa dawa na tiba kwa gharama nafuu UNITAID leo limeendelea na ziara yake kukagua faida za miradi bunifu ya kuimarisha sekta ya afya ambayo imeboresha maisha ya maelfu ya wakenya na wakati huo huo kuokoa fedha.

Herve Verhoosel ambaye ni msemaji wa shirika hilo tanzu la lile la Umoja wa Mataifa la afya, WHO akizungumza kutoka Nairobi, Kenya amesema “kwa ushirikiano na Kenya, UNITAID imeanzisha matumizi ya vipimo vya mapema vya Virusi Vya Ukimwi kwa watoto, dawa bora za kupunguza makali ya Ukimwi kwa watoto, dawa rafiki kwa watoto dhidi ya Kifua Kikuu, uchunguzi wa kisasa na tiba dhidi ya saratani ya shingo ya kizazi, chanjo mpya ya Malaria na ufikiaji rahisi wa uchunguzi na tiba dhidi ya coronavirus">COVID-19.”

Watoto wanahudhuria kikao cha uhamasishaji kuhusu FGM huko Katiola, Côte d'Ivoire.
© UNICEF/Olivier Asselin
Watoto wanahudhuria kikao cha uhamasishaji kuhusu FGM huko Katiola, Côte d'Ivoire.

FGM

Ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya kutokomeza ukeketaji wa wanawake na watoto aw kike, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres kwenye ujumbe wake amesema mwaka huu wa 2024 wasichana milioni 4.4 wakiwa hatarini kukeketwa kila mtu achukue hatua maradufu kuepusha kitendo hicho ambacho kinakiuka haki za msingi wa binadamu na kusababisha machungu ya afya ya mwili na akili kwa wanawake na wasichana.

Guterres amesema inahitaji hatua za kimsingi kushughulikia maadili ya kijamii, kiuchumi na kisiasa yanayosongesha ubaguzi dhidi ya wanawake na wasichana na kuzuia ustawi wao kielimu na kwenye ajira.