Baraza Kuu la UN laiongezea haki Palestina, lakini bado si mwanachama kamili wa UN
Hii leo Baraza kuu la Umoja wa Mataifa -UNGA limepitisha azimio namba A/ES-10/L.30/Rev.1. la kuongezea taifa la Palestina haki ndani ya Baraza hilo, haki ambazo nchi nyingine 193 wanachama wanazo ndani ya Baraza hili, ingawa halitapata haki ya kupiga kura ndani ya chombo hicho cha ngazi ya juu cha maamuzi cha Umoja wa Mataifa.