Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ICCAO Tanzania: Shirika la vijana linalosaidia kufanikisha SDGs nchini Tanzania

Zahra K Salehe Mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji, ICCAO Tanzania akizungumza na wanafunzi.
UN News
Zahra K Salehe Mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji, ICCAO Tanzania akizungumza na wanafunzi.

ICCAO Tanzania: Shirika la vijana linalosaidia kufanikisha SDGs nchini Tanzania

Malengo ya Maendeleo Endelevu

Mnamo tarehe Mosi Januari mwaka 2016, Malengo 17 ya Maendeleo Endelevu (SDGs) yalianza kufanyiwa kazi rasmi. Tangu wakati huo watu ulimwenguni kote kwa ngazi tofautifauti wamekuwa wakihaha kuhakikisha kufikia mwaka 2030 malengo hayo yanafikiwa. Na kila mara Makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani yamekuwa uwanja wa wazi kwa wadau kutoka kila pembe ya dunia kuja katika mikutano mbalimbali na kubadilishana uzoefu. 

Mfano ni Mkutano wa 68 wa Kamisheni ya Hali ya wanawake duniani, CSW68 ulifanyika hivi karibuni na mmoja wa waliohudhuria ni huyu ambaye katika mahojiano haya na Anold Kayanda wa Idhaa hii tunapata kufahamu baadhi ya malengo yanavyotekelezwa na shirika lake nchini Tanzania.