Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Habari Mpya

Mgonjwa wa TB akiwa anaendelea na matibabu nyumbani  nchini Colombia.
© PAHO/Joshua Cogan

Viongozi wa dunia na ahadi mpya ya kutokomeza TB

Vifijo na nderemo vilisikika kwenye moja ya kumbi za mikutano kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani hii leo baada ya wawakilishi wa serikali, wataalamu wa afya na wawakilish iwa mashirika ya kiraia kupitisha azimio la kisiasa lenye lengo la kutokomeza Kifua Kikuu au TB ifikapo mwaka 2030 ambapo pamoja na mambo mengine linalenga kufikia asilimia 90 ya watu na huduma za kinga na tiba dhidi ya TB.

Chini ya nusu ya Nchi Zilizoendelea na chini ya theluthi moja pekee ya Nchi Zinazoendelea za Visiwa Vidogo zina mfumo wa maonyo ya mapema.
© UNDRR/Amir Jina

Nchi zilizo katika bonde la mto Nile kunufaika na mradi wa tahadhari za mapema

Maji yakiwa mengi yanaweza kusababisha mafuriko kama yaliyotokea hivi karibuni huko nchini Libya na uwepo wa maji kidogo unaweza kusababisha ukame kama hali ilivyo kwa nchi nyingi za ukanda wa Jangwa la Sahara kwa sasa, na ndio maana wadau wa masuala ya hali ya hewa wametaka suala la maji kuwa kitovu wakati dunia inashughulikia mabadiliko ya tabianchi. 

Waziri wa Afya wa Kenya Susan Nakhumicha Wafula.
UN News

Kama COVID-19 ilivyotiliwa mkazo ifanyike hivyo kwa Kifua Kikuu

Mkutano wa ngazi ya juu kuhusu mapambano dhidi ya kifua kikuu au TB ukifanyika leo hapa katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York Marekani, Waziri wa Afya wa Kenya Susan Nakhumicha Wafula amesema kutokomeza TB ifikapo mwaka 2030 inawezekana endapo Dunia itashikama na kuweka msokumo mkubwa kwa ugonjwa huo kama ilivyofanya wakati wa mlipuko wa janga la COVID-19.

Sauti
2'7"
Jessica Alupo Makamu wa Rais wa jamhuri ya Uganda akihutubia mjadala mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa  UNGA78
UN Photo/Cia Pak

Nchi zinazoendelea zihusishwe katika maamuzi ya mageuzi ya mifumo ya fedha:Uganda

Uganda imekuwa mstari wa mbele katika ukarimu wa kupokea na kukumbatia wimbi kubwa la wakimbizi  kutoka ndani ya kanda na hata imeorodheshwa kama moja ya nchi inayopokea na kuhifadhi wimbi kubwa la wakimbizi duniani. Hivyo ndivyo alivyoanza hotuba yake makamu wa Rais wa Uganda Jessica Alupo alipohutubia mjadala mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa jioni ya leo jijini New York Marekani.

Makamu wa Rais wa Tanzania, Philip Isdor Mpango akihutubia katika mjadala mkuu wa Mkutano wa 78 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, New York, Marekani. (21 Sept 2023).
UN Photo/Cia Pak

‘Jicho kwa jicho, huacha kila mtu kipofu’ – Makamu wa Rais wa Tanzania katika UNGA 78

Msemo wa wahenga, “Jicho kwa jicho huacha kila mtu kipofu” umepata nafasi katika ukumbi maarufu wa kihistoria wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa nchini Marekani pale ambapo Makamu wa Rais wa Tanzania, Dkt. Philip Isdor Mpango ameutumia msemo huo akisisitiza amani ulimwenguni alipohutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa saa za jioni jijini New York.