Mwaka 2022 tuazimie kujikwamua kutoka majaribuni- Guterres
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres ametuma salamu za mwaka mpya wa 2022 akitaka dunia iazimie kwa pamoja mwaka huu mpya uwe wa kuondokana na majaribu yanayotarajia kuikumba.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres ametuma salamu za mwaka mpya wa 2022 akitaka dunia iazimie kwa pamoja mwaka huu mpya uwe wa kuondokana na majaribu yanayotarajia kuikumba.
Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR limesikitishwa na vifo vya hivi karibuni vya watu 31 waliokufa maji katika matukio matatu tofauti ya kuzama kwa boti kwenye bahari ya Aegean.
Nchini Cote d’Ivoire shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR limeleta tabasamu na nuru kwa wakimbizi ambao biashara zao zilivurugika kutokana na janga la ugonjwa wa Corona au COVID-19 ambalo limetikisa dunia kuanzia mwaka jana wa 2020. Kwa sasa wakimbizi hao wakiwemo wa kutoka Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, DRC wana imani ya kujiinua tena kiuchumi.
Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo, FAO Qu Dongyu ametoa ujumbe wake kwa mwaka mpya wa 2022 huku akitaja mafanikio ambayo shirika hilo limefanikisha mwaka huu wa 2021 licha ya changamoto ya janga la ugonjwa wa Corona au COVID-19.
Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, MINUSCA, tarehe 25 Desemba mwaka huu umeanzisha operesheni ya kuwatimua wanakundi takribani 200 wa kundi linalojihami kwa silaha la Unity for Peace in Central Africa, UPC kutoka mji wa Boyo, mkoani Ouaka.
Taarifa iliyotolewa na Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia, UNSOM hii leo mjini Mogadishu, Somalia imeeleza kwamba wadau wa kimataifa wanafuatilia kwa wasiwasi mkubwa hali ya sasa na maendeleo ya kisiasa nchini Somalia.
Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani MONUSCO umelaani vikali shambulio lililofanyika siku ya krismasi na kusababisha vifo vya watu wanane.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema janga la COVID-19 limedhihirisha ni jinsi gani magonjwa ya kuambukiza yanavyoweza kuzuka haraka na kusambaa kote duniani, kutoa shinikizo kubwa kwenye mifumo ya afya na kupindua maisha ya watu kwa binadamu wote.
Mamlaka nchini Myanmar lazima zichunguze shambulio hatari la hivi karibuni dhidi ya raia kwenye jimbo la Kayans, amesema hii leo Mkuu wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya uratibu wa misaada ya dharura, OCHA Martin Griffiths.
Umoja wa Mataifa umelaani kitendo cha uporaji na ghasia katika kilichokuwa kituo cha ujumbe wa pamoja wa Umoja wa Mataifa na Muungano wa Afrika, AU wa kulinda amani huko Darfur nchini Sudan, UNAMID.