Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Habari Mpya

Wahudumu wa kiafya katika hospitali ya tiba ya Chuo Kikuu cha Nanjin nchiin china wakishauriana na mgonjwa kuhusu upasuaji wa kupandikiza pafu.
Chen Jingyu

Virusi vilivyotikisa dunia: 2020, mwaka tofauti na mingine

Ugonjwa unaosababishwa na virusi vya Corona au COVID-19 uko kila pahali na katika mwaka 2020 ulisambaa na kuleta madhara makubwa yaliyosababisha janga la dunia ambalo mapana yake hayakutarajiwa. Katika mfululizo wa makala sita juu ya mwaka huu wa mtikisiko, UN News inamulika athari za ugonjwa huu kwa watu kwenye maeneo mbalimbali ya dunia na suluhisho ambazo Umoja wa Mataifa umependekeza kufuatia janga hili. Katika makala hii ya kwanza tunamulika mambo ya msingi katika miezi 12 ya mwaka huu wa 2020.