Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Habari Mpya

Ofisa wa Habari wa UNMIS asailia mpango wa amani kwa Darfur

Jumbe Omari Jumbe, Ofisa wa Habari wa Shirika la UM juu ya Ulinzi wa Aamani Sudan (UNMIS) anatuchambulia fafanuzi zake kuhusu juhudi za wapatanishi wa kimataifa juu ya Darfur, yaani Jan Eliasson wa Umoja wa Mataifa na Salim Ahmed Salim akiwakilisha Umoja wa Afrika. Wapatanishi Eliasson na Salim walikuwepo Sudan wiki hii kujaribu kufufua tena mazungumzo ya kusuluhisha mzozo wa Darfur kwa ridhaa ya makundi yote husika.~~Sikiliza idhaa ya mtandao kwa mahojiano kamili na Jumbe.

Ofisa wa Habari wa UNMIS asailia mpango wa amani kwa Darfur

Jumbe Omari Jumbe, Ofisa wa Habari wa Shirika la UM juu ya Ulinzi wa Aamani Sudan (UNMIS) anatuchambulia fafanuzi zake kuhusu juhudi za wapatanishi wa kimataifa juu ya Darfur, yaani Jan Eliasson wa Umoja wa Mataifa na Salim Ahmed Salim akiwakilisha Umoja wa Afrika. Wapatanishi Eliasson na Salim walikuwepo Sudan wiki hii kujaribu kufufua tena mazungumzo ya kusuluhisha mzozo wa Darfur kwa ridhaa ya makundi yote husika.~~Sikiliza idhaa ya mtandao kwa mahojiano kamili na Jumbe.

CERF yaifadhilia WFP dola 600,000 kuhudumia chakula wakazi wa Ogaden

Taasisi inayosimamia Mfuko Maalumu wa UM Kuhudumia Maafa ya Dharura (CERF) imelifadhilia Shirika la Miradi ya Chakula Duniani (WFP) dola 600,000 kuwapatia chakula raia wa Ethiopia wenye asili ya KiSomali wanaoishi kwenye eneo lilioshuhudia mfumko wa mapigano makali karibuni baina ya vikosi vya Serikali na Kundi la Ukombozi wa Ogaden.

Watu 500,000 waling'olewa makwao mwaka jana DRC, UM yathibitisha

Ofisi ya UM juu ya Misaada ya Dharura (OCHA) imeripoti kwamba katika miezi 12 iliopita watu nusu milioni waling’olewa makwao katika Jamhuri ya Kidemokrasiya Kongo (DRC) kwa sababu ya kuselelea kwa mapigano baina ya Jeshi la Taifa (FARDC) na makundi ya waasi na wanamgambo, hali ambayo haijawahi kushuhudiwa tangu 2003 pale vita vya wenyewe kwa wenyewe viliposhtadi kwa wingi nchini humo.

UM wahudumia juhudi kinga dhidi ya gharika Msumbiji

Timu ya Wafanyakazi Wakazi wa UM Wanaohudumia Misaada ya Kiutu wameripotiwa kushiriki kikamilifu hivi sasa kwenye operesheni za kuisaidia serikali ya kijiji katika Caia, nchini Msumbiji kudhibiti bora huduma za dharura, baada ya kuzuka maafa yaliotokana na mafuriko ambayo huhatarisha zaidi hali za wale wakazi wanaoishi kwenye maeneo yaliopo karibu na Mto Zambezi.

UNICEF kuiombea Malawi msaada wa dharura kudhibiti mafuriko

Shirika la UM kuhusu Mfuko wa Maendeleo kwa Watoto (UNICEF)limetangaza ombi maalumu linaloishinikiza jumuiya ya kimataifa kufadhilia mchango wa dharura wa dola milioni 2.5 kuhudumia chakula ule umma ulioathirika na mafuriko yaliosambaa Malawi. UNICEF imetahadharisha kwenye taarifa yake kwamba pindi ombi lao halitokamilishwa kwa wakati kuna hatari ya watu milioni moja kukabiliwa na njaa maututi katika Malawi.

Operesheni za UNOCI zaongezewa miezi sita Cote d'Ivoire

Baraza la Usalama limepitisha kwa kauli moja azimio la kuidhinisha operesheni za ulinzi wa amani ziendelezwe kwa miezi sita zaidi hadi 30 Julai katika Cote d\'Ivoire, huduma ambazo husimamiwa na kuongozwa na shirika la UM la UNOCI pamoja na wanajeshi wa Ufaransa. , ongeza kwa miezi sita muda wa operesheni za ulinzi wa amani za Shirika la UM la UNOCI katika Cote d’Ivoire.

Mjumbe Mpya wa UM kwa Liberia amewasili kuanza kazi

Mjumbe Maalumu mpya wa KM kwa Liberia, Ellen Margrethe Loj wa Denmark amewasili Liberia kuanza kazi, na aemahidi kulisaidia taifa husika la Afrika Magharibi kuimarisha amani, utulivu na demokrasia katika kipindi cha mpito baada ya vita vya wenyewe kwa wenyewe vya miaka kumi kusitishwa nchini. ~~Bi Loj alisema ijapokuwa mafanikio kadha yameshuhudiwa baada ya mapigano kusita, hata hivyo badio kuna majukumu mbalimbali yanayohitajia kushughulikiwa kuupatia umma wa Liberia utulivu wanaohitajia kuendeleza maisha yao ya kawaida.