Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

KM atateua tume huru kuchunguza shambulio la ofisi za UM Algiers

KM atateua tume huru kuchunguza shambulio la ofisi za UM Algiers

David Veness, Mshauri Mkuu anayehusika na Masuala ya Ulinzi na Usalama katika UM aliripotiwa kumkabidhi KM Ban Ki-moon ripoti ya utangulizi kuhusu sababu zilizochochea shambulio la ugaidi kwenye ofisi za UM ziliopo Algiers, Algeria, ajali ambayo ilijiri mwezi uliopita.