Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

CERF yaifadhilia WFP dola 600,000 kuhudumia chakula wakazi wa Ogaden

CERF yaifadhilia WFP dola 600,000 kuhudumia chakula wakazi wa Ogaden

Taasisi inayosimamia Mfuko Maalumu wa UM Kuhudumia Maafa ya Dharura (CERF) imelifadhilia Shirika la Miradi ya Chakula Duniani (WFP) dola 600,000 kuwapatia chakula raia wa Ethiopia wenye asili ya KiSomali wanaoishi kwenye eneo lilioshuhudia mfumko wa mapigano makali karibuni baina ya vikosi vya Serikali na Kundi la Ukombozi wa Ogaden.

WFP imeshapeleka tani za metriki 17 kwenye kanda tano zilizovamiwa na operesheni za kivita. Hata hivyo, kwa sababu ya ukosefu wa ulinzi wa wanajeshi wa kushindikiza misafara ya chakula, inayotakikana kwenye maeneo ya uhasama, misaada hii mara nyingi hucheleweshwa kuwafikia wale raia muhitaji kwa wakati.