Hatua mliyochukua kamati ya katiba ya Syria ni matumaini kwa wasyria wote- UN
Umoja wa Mataifa umesema hatua iliyochukuliwa na kamati ya katiba ya Syria kwa mara ya kwanza kuwakutanisha uso kwa uso serikali ya nchi hiyo na tume ya upinzani ya majadiliano na pia asasi za kiraia ni hatua kubwa na muhimu kuelekea mustakabali wa taifa hilo.