Kazi ni kazi bora mkono wende kinywani:Mkimbizi Amina

Wakimbizi kutoka Syria wakiwa kambini Domiz nchini Iraq
OCHA
Wakimbizi kutoka Syria wakiwa kambini Domiz nchini Iraq

Kazi ni kazi bora mkono wende kinywani:Mkimbizi Amina

Wahamiaji na Wakimbizi

Hakuna kazi mbaya ili mradi haikulazi njaa wewe na familia yako, hiyo ni kauli ya Bi. Amina mkimbizi kutoka Syria ambaye kwa sasa anaishi kwenye kambi ya wakimbizi ya Domiz akifanya kila awezalo kulisha familia yake kwa msaada wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR. 

Kambini Domiz nchini Iraq ni Bi., Amina akiendelea kushona nguo katika jerahani yake anasema “naipenda kazi yangu na nataka kuwa fundi cherahani maarufu na mbobevu”.

Mkimbizi huyo kutoka Syria aliachwa mjane akiwa na umri mdogo wa miaka 39 tu, ana watoto saba na wajukuu watatu, anatumia ujuzi wake wa mitindo na kushona ili kuhakikisha familia na biashara yake sio tu inaendelea bali inashamiri kambini Domiz, “najaribu kila wakati kujiendeleza.Naangalia mitindo mipya kwenye intaneti na kujaribu kwenda na mienendo mipya.”

Ubunifu wake umempa fursa kubwa, alianza na kiduka kidogo lakini sasa biashara yake shamiri na yenye mafanikio, leo hii anashona nguo za mitindo mbalimbali kwa ajili ya wakimbizi, wateja kutoka nje na jamii zinazowahifadhi.

Amejikita zaidi katika mitindo ya nguo za wanawake na magauni ya harusi lakini pia anajitolea katika kituo cha mafunzo cha UNHCR kuwafundisha wakimbizi wengine na wanawake wa eneo la Domiz kushona nguo. Miongoni mwa wanafunzi wake ni Shahinaz, “ametufundisha jinsi ya kushona nguo za watoto, nguo za kiasili za Wakurdi na magauni marefu”

Amina anasema hata kama hawaweza kufungua duka kama mie lakini wakifanyakazi kwenye viwanda au makampini basi watakuwa na ujasiri.

Katika kambi ya Domizi kwa mujibu wa UNHCR kuna wakimbizi wa Syria zaidi ya 32,390 na wengi walikimbia Syria vita vilipozuka 2011.