Somalia imepiga hatua lakini jitihada zaidi zahitajika kukomesha ukatili dhidi ya wanawake:De Clercq
Nchini Somalia leo kumezinduliwa kampeni ya siku 16 za uhamasishi kupinga ukatili dhidi ya wanawake ambapo Umoja wa Mataifa umetoa wito kwa sekta zote za jamii nchini humo kuchukua hatua madhubuti kusaidia kukomesha ukatili huo.