Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wahusika wa shambulio la kigaidi Somalia wawajibishwe:Baraza

Magari  yaliyoharibika kufuatia mashambulio mawili ya kujilipua yaliyofanywa na Al Shabaab nchini Somalia na kusababisha vifo vya makumi kadhaa ya watu.
UN /Stuart Price
Magari yaliyoharibika kufuatia mashambulio mawili ya kujilipua yaliyofanywa na Al Shabaab nchini Somalia na kusababisha vifo vya makumi kadhaa ya watu.

Wahusika wa shambulio la kigaidi Somalia wawajibishwe:Baraza

Amani na Usalama

Wanachama wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wamelaani vikali shambulio la kigaidi la Novemba 9 mjini Mogadishu nchini Somalia ambalo limesababisha raia wengi wasio na hatia kufariki dunia na wengine kujeruhiwa.

Katika taarifa iliyotolewa jumamosi mjini New York, Marekani kuhusu shambulio hilo, wanachama wa Baraza la Usalama wametoa rambirambi zao kwa familia za waathirika pamoja na watu na Serikali ya Somalia na kuwatakia afueni ya haraka wote waliojeruhiwa. Vilevile wamepongeza jinsi wafanyakazi ya huduma ya kwanza na serikali walivyoitukia kusaidia majeeuhi na waliopoteza maisha katika shambulio hilo.

Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali vya habari, kundi la wanamgambo la Al Shabab ndilo limedai kuhusika na shambulio hilo lililokatili takriban maisha ya watu 20 na kujeruhi zaidi ya mia moja, wakati gari lililokuwa limejaa vilipuzi kulipka nje ya hoteli moja mjini Mogadishu . Al Shabab wanaipinga serikali ya sasa nchini Somalia na mara kadhaa wamehusika katika mashambulizi ya kigaidi.

Wajumbe wa baraza pia kuonya kwamba ugaidi wa aina yoyote ile bado ni tisho kubwa kwa amani na usalama duniani na kusisitiza haja ya kuwachukulia hatua za kisheria wahusika, watayarishaji, wafadhili wa visa vya kigaidi na kuhimiza mataifa yote, kutekeleza wajibu wao chini ya sheria za kimataifa na maazimio ya baraza la usalama, kusirikina vilivyo na serikaliya Somalia na pia wakuu wote husika katika jukumu hili.