Tuzingatie changamoto Somalia kabla ya kuondoa vikosi vya AMISOM:Nyanduga 

29 Oktoba 2018

Hatua ya kupunguza vikosi vya Muungano wa Afrika vinavyolinda amani nchini Somalia ni nzuri kwa muktada wa kuipa jukumu serikali ya shirikisho katika masuala ya usalama wa taifa lake, lakini inapaswa kuzingatia changamoto zilizopo.

Tahadhari hiyo imetolewa na mtaalamu huru wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu nchini Somalia, Bahame Tom Nyanduga alipozungumza na Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa mjini New York Marekani kandoni mwa vikao vya kamati ya tatu ya Baraza kuu vinavyosikiliza ripoti za wataalamu mbalimbali wa haki za binadamu.

Akihimiza hoja hiyo kwa kuzingatia misingi ya haki za binadamu Bwana. Nyanduga amesema

Tarehe 30 Julai mwaka huu Baraza la Usalama lilipitisha azimio la kutaka vikosi vya muungano wa Afrika vinavyolinda amani nchini Somalia , AMISOM kupunguza idadi ya vikosi nchini humo ifikapo Mei 2019. Nyanduga amesema ili hatua hiyo ifanikiwe bila zahma yoyote kwa watu na taifa la Somalia ambalo kwa karibu miongo mitatu liko kwenye machafuko kuna

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud