Miaka 20 ya azimio namba 1325: Mafanikio na Changamoto
Mwaka huu azimio namba 1325 la Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kuhusu wanawake na ulinzi na usalama duniani, limetimiza miaka 20 tangu kupitishwa kwake.
Mwaka huu azimio namba 1325 la Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kuhusu wanawake na ulinzi na usalama duniani, limetimiza miaka 20 tangu kupitishwa kwake.
Leo ni kumbukumbu ya miaka mitatu tangu kufanyika kwa shambulio kubwa zaidi la kigaidi mjini Moghadishu Somalia mnamo 14 Oktoba 2017.
Kamati ya tuzo ya amani ya Nobel yenye makao yake nchini Norway leo imelitangaza shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP kuwa ndio mshini wa tuzo ya amani ya Nobel kwa mwaka huuu wa 2020.
Malaki ya watoto nchini Somalia wamechanjwa dhidi ya ugonjwa wa surua na polio wakati wa kampeni ya chanjo kudhibiti mlipuko wa magonjwa hayo hatari, imeeleza taarifa ya mpango wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia, UNSOM.
Rais wa Somalia Mohamed Abdullahi Mohamed Farmajo hii leo akihutubia mjadala wa wazi wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kwa njia ya video iliyorekodiwa, amesema wanaendelea kushirikiana na Umoja wa Mataifa na wadau wengine katika masuala mbalimbali ili kutengeneza mstakabali mzuri kwa watu wa Somalia.
Mashirika ya Umoja wa Mataifa yametoa mwongozo wenye mapendekezo ya mikakati ya kiafya ya kuzingatiwa na serikali kuhusu linin a jinsi ya kufungua tena shule kwenye maeneo ambako shule bado zimefungwa kutokana na janga la ugonjwa wa Corona au COVID-19.
Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR limesema janga la ugonjwa wa Corona, au COVID-19 ni tishio kubwa kwa elimu ya wakimbizi duniani kote.
Janga la ugonjwa wa virusi vya Corona au COVID- 19 likiendelea kuripotiwa maeneo mbalimbali duniani, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametoa tamko lake la kisera lenye lengo la kuhakikisha kuwa janga hilo halizidishi pengo lililokuwa la walio na elimu na wasio na elimu.
Mwakilishi maalum wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia James Swan ameipongeza serikali ya Somalia kwa juhudi kubwa inazozifanya katika upimaji wa virusi vya corona au COVID-19 baada ya leo kuzuru maabara ya taifa ya afya ya umma (NPHRL) mjini Moghadishu.
Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na mkuu wa mpango wa Umoja huo nchini Somalia UNSOM, James Swan amesema msaada uliotolewa na wadau wa kimataifa umeisadia Somalia kuweka kituo kwa ajili ya huduma kwa wagonjwa wa corona au COVID-19, na kuwataka wadau hao kuongeza msaada zaidi kwa serikali.