Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

DR Congo

Dikembe Mutombo, Rais wa Mfumo wa Dikembe Mutombo na pia mcheza kikapu mashuhuru wa NBA ambaye sasa amestaafu. Pichani akiwa katika vikao maalum kwenye makao makuu ya UN kuhusu uzuiaji uhalifu, Aprili 2018
UN /Manuel Elias

E4J ndio mwelekeo wa kunusuru vijana - Mutombo

Balozi wa kimataifa wa chama cha mpira wa kikapu nchini Marekani,  NBA, Dikembe Mutombo amesema kuwapatia vijana elimu inayowawezesha kujiepusha na vitendo vya uvunjifu wa amani ni suala mujarabu katika kutekeleza lengo namba 16 la malengo ya maendeleo endelevu, SDGs linalohusu amani, haki na taasisi thabiti.

Sauti
1'52"
Taswira ndani ya Baraza Kuu wakati wa upigaji kura wa azimio namba 2439 kuhusu Ebola nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, DRC leo tarehe 30 Oktoba 2018
UN /Manuel Elias

Baraza la Usalama lapitisha azimio kuchagiza harakati dhidi ya Ebola DRC

Hii leo kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa wajumbe wa Baraza la Usalama kwa kauli moja wamepitisha azimio ambalo pamoja na kuchagiza harakati za kukabiliana na ugonjwa wa Ebola nchini  Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC , limelaani vikali mashambulizi na mauaji  ya watoa huduma za afya ambao wanaweka rehani maisha yao kutokomeza ugonjwa huo hatari.

Sauti
3'6"